ABWENE MWASONGWE NI MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI ANAYE ELEZEA UHALISIA WA MTU ANAVYOKUWA NA IMANI.
MUIMBAJI HUYU WA NYIMBO ZA INJILI ABWENE MWASONGWE AMETOA CD TATU , NA HII YA TATU NI MISULI YA IMANI.
Abwene ni kijana mwenye umri wa miaka 28 na ni mwanafunzi wa chuo kilichopo Mbeya anaye somea mambo ya uhasibu na hajaoa bado lakini mungu hajamuacha amempa kipaji cha kuimba nyimbo za injili zenye kubeba ujumbe na ushuhuda wa maisha yetu.Abwene amesema kuwa aliamua kuipa albamu yake jina hilo kutoka na kisa ama ushuhuda ambao ameuimba katika wimbo huo wa mama aliyekuwa na watoto saba na wote wakafa siku moja.kuna watu ambao mara nyingi hawaamini katika dunia ya leo kama ilivyo kuwa kwa Ayubu ambaye mateso yake yanajulikana kwa kila msomaji wa bibilia .Hayatofautiani sana na huyu aliyefiwa na watoto saba kwa siku moja hali ambayo inatia sana uchungu na pengine unaweza ukamwacha mungu na kwenda kwa waganga wa kienyeji,lakini huyu mama alikuwa na "misuri ya imani"wala hakumtenda mungu wake dhambi aliweza kuhimili shida zake kwa kupiga magoti na kumuomba mungu wake aliye hai wakati wote wala hashindwi.
MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI ABWENE MWASONGWE ALIYEJAZWA ROHO MTAKATIFU.
Hivyo Abwene anaendelea kusema maana ya wimbo huo wa "misuri ya imni" ni kuwaeleza watu jinsi imani inavyotenda kazi namna watu wanavyotakiwa kumuimini mungu katika shida raha. kwa kupitia wimbo huo unaweza ukampokea mungu awe ndani yako.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni